Shughuli ya usambazaji karatasi za kupigia kura ya ugavana katika Kaunti ya Mombasa imeanza huku mipango yote ikikaribia kukamilika.
Mapema leo hii masanduku ya kupigia kura yalifunguliwa ili kuthibitisha karatasi hizo inatekelezwa chini ya uangalizi wa maajenti wa wawaniaji wote 7 wa Ugavana wa Mombasa pamoja na wawaniaji wenyewe.
Baadaye wasimamizi wa vituo vyote 1,037 pamoja na manaibu wao watakabidhiwa vifaa hivyo vya kupigia kura.