Shughuli ya kuwahoji mawaziri wateule inaanza rasmi Jumatatu huku kizungumkuti kikiwa kimezingira uteuzi wa Musalia Mudavadi kuwa Mkuu wa Mawaziri. Katika ratiba ya mahoajiano hayo yatakayoanza Jumatatu hadi Jumamosi ijayo Mudavadi ndiye ameratibiwa kufika wa kwanza, hata hivyo, kabla ya kuhojiwa Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetangula atasubiriwa kutoa mwelekeo kuhusu nafasi hiyo.
Wiki iliyopita Spika Wetangula alisema atatoa mwelekeo huo Jumatatu asubuhi kabla ya shughuli ya kuanza kuwahoji mawaziri wateule kuanza mwendo wa saa tatu. Hatua hii inafuatia mvutano maswali yaliyoibuliwa na upande wa wachache bungeni kuhusu nafasi aliyotengewa mudavadi ukisema haitambuliki kikatiba.