Kampuni ya Safaricom imezindua kampeni mpya kwa jina ''Tuinuane'' inayolenga kuwapa Wakenya moyo wa kusaidiana.
Chini ya Kampeni hiyo Safaricom inalenga kuiwezesha jamii kwa kuhakikisha wanafunzi wanapata vifaa vya masomo kwa haraka kando na kuzindua huduma mpyana za kisasa kwa manufaa ya wateja wake.
Afisa Mkuu Mtendani wa Safaricom Peter Ndegwa amesema kampeni ya ''Tuinuane'' imetokana na moyo wa Wakenya wote wa kujitolea kutoa usaidizi.
Chini ya Mpango huo, Wakfu wa Safaricom kupitia mpango wa Ndoto Zetu itaimarisha ushirikiano wake na jamii.