×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Mwenyekiti wa IEBC apokonywa mamlaka

News

Mahakama ya Upeo umeondoa mamlaka ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi IEBC ya kuthibitisha, kujumlisha na kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa Urais.

Katika uamuzi wao, Majaji hao saba wakiongozwa na Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu wake Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung'u, Isaac Lenaola vilevile William Ouko wamefafanua kwamba jukumu hilo ni la makamishna wote saba wa IEBC na wala si la mwenyekiti pekee.

Uamuzi huo aidha umekitaja Kipengele cha themanini na saba ibara ya tatu cha sheria za uchaguzi mkuu cha mwaka 2012 kinachompa mamlaka ya kuthibitisha, kujumlisha na kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa urais Mwenyekiti wa IEBC bila kuwapo kwa makamishna wengine kuwa kinyume na katiba.

Aidha majaji hao wamesema Mwenyekiti anajukumu la kipekee baada ya kuthibitishwa na kujumlishwa kwa matokeo na makamishna wengine kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa urais, na kwamba mgawanyiko uliokuwapo baina ya Chebukati na makamishna wenzake Juliana Cherera, Irene Masit, Francis Wanderi na Justus Nyangaya haukuathiri kivyovyote vile matokeo ya uchaguzi wa urais.

Jopo hilo aidha limependekeza bunge kulainisha baadhi ya majukumu ya maafisa wa IEBC vilevile sera za utendakazi wa maafisa hao ili kuepuka mgogoro kwenye chaguzi zijazo.Kuhusu teknolojia wakati wa uchaguzi, majaji hao wameagiza IEBC kuhakikisha inazilinda sava zake na kwamba wanaozifikia fomu za 34A, 34B na 34C wawe maafisa wake pekee vilevile kuongezwa kwa sehemu kwenye fomu 34A inayoonesha idadi ya kura zilizoharibika.Vilevile majaji hao wamemkinga Chebukati dhidi ya kuwajibishwa kwa makosa ya uhalifu katika matokeo hayo ya uchaguzi yaliyokumbwa na utata na kulitupilia mbali ombi la Raila Odinga na Martha Karua la kuitaka Mahakama kumtaja kuwa asiyefaa kushikilia wadhifa wowote wa umma.Kulingana nao, madai dhidi ya Chebukati hayakuwa na uzito wa kufanikisha maombi ya walalamishi katika rufaa hiyo ya kumwondoa ofisini kwa vile mchakato huo umefafanuliwa na katiba kwenye kipengele cha 251.

Related Topics


.

Popular this week

.

Latest Articles