×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]

Mwamba wa lugha: Udadavuzi wa ngeli ya A - WA

News
 Geoffrey Mung'ou [Photo: Courtesy]

Ngeli ni kundi la nomino zenye sifa zinazofanana kisarufi. Nomino za A-WA zina kiambishi ‘a’ cha umoja na ‘wa’ cha wingi, katika upatanisho wa kisarufi.

Mfano katika sentensi: Mwanafunzi amefika shuleni - Wanafunzi wamefika shuleni.

Ngeli ya A-WA hujumuisha majina ya:

i. Wanadamu. Mifano: mtoto na shangazi.

ii. Wanyama. Mifano: ng’ombe na mbuzi.

iii. Ndege. Mifano: kuku na kipanga.

iv. Viumbe wa majini. Mifano: dagaa na papa.

v. Wadudu. Mifano: sisimizi na kereng’ende.

vi. Kiimani au matakatifu. Mifano: Maulana na Mtume Mohammed.

vii. Viumbe wasababishao zahama, kama vile pepo na shetani.

 Miundo ya Ngeli ya A-WA

Kwa mujibu wa Mwamba wa Sarufi na Mung’ou G. (2018) uk.71-73, kuna miundo ifuatayo ya majina ya ngeli ya A-WA:

(a) m-wa. Unahusu nomino zenye kiambishi ‘m-’ mwanzoni katika umoja na ‘wa-’ katika wingi. Mifano: mtakatifu-watakatifu, mtu-watu.

Mfano katika sentensi: Mchezaji huyu ni stadi - Wachezaji hawa ni stadi.

(b) mw-w. Unahusu nomino zenye kiambishi ‘mw-’ mwanzoni, katika umoja na ‘w-’ katika wingi. Mfano: mwizi - wezi.

(c) m-mi. Unahusu nomino zenye kiambishi ‘m-’ katika umoja na ‘mi-’ katika wingi. Mifano ni mkunga –mikunga, mkizi –mikizi.

Mfano katika sentensi: Mkunga amevuliwa - mikunga wamevuliwa. (aina ya samaki)

(d) mu-wa. Muundo huu unahusu nomino zenye kiambishi ‘mu-’ katika umoja na ‘wa-’ katika wingi. Mifano: Muungwana - waungwana, mutribu - watribu.

(e) ki-vi. Muundo huu unahusu nomino zenye kiambishi ‘ki-’ katika umoja na ‘vi-’ katika wingi. Mfano: kipepeo - vipepeo.

(f) ch-vy. Mfano chura - vyura (‘ch-’ katika umoja na ‘vy-’ katika wingi).

Mfano katika sentensi: chura ametoka majini – vyura wametoka majini.

(g) ‘Ø-ma. Unahusu nomino zenye umbo kapa (lisilodhihirisha viambishi katika umoja), ila zina kiambishi ‘ma-’ katika wingi. Mifano ni karani - makarani na askofu - maaskofu.

Mfano katika sentensi: Askofu ametawazwa - Maaskofu wametawazwa.

(h) Muundo kappa (Ø-Ø). Muundo huu unahusu majina yenye maumbo yasiyobadilika katika umoja na wingi. Nomino zenye muundo huu:

i. Zina kiambisha ‘a-’ cha upatanisho wa kisarufi ambacho hakibadiliki katika wingi. Mifano: Mungu na Yesu.

Mfano katika sentensi: Mungu ameniokoa – Mungu ametuokoa.

ii. Zina kiambishi ‘a-’ cha umoja na ‘wa-’ cha wingi. Mifano: simba na ndovu.

Mfano katika sentensi: Simba anatisha –simba wanatisha.

 [email protected]

[email protected]

 DIBAJI ZA WALLAH BIN WALLAH

1. Usiupoteze wakati asubuhi ukaja kuutafuta jioni. Hutaupata.

2. Usimlaumu Mungu kwa makosa yako; ujilaumu mwenyewe.

3. Ukiandika kitabu, umewaachia watu elimu ya milele.

4. Pigana na uzembe wako, usipigane na juhudi za watu wengine.

5. Simba si paka. Hata kama amelala, usimchokoze.

Maneeeeno hayo!

 

 

 

 

 

Related Topics


.

Popular this week

.

Latest Articles