Juma lililopita tulianza kuzungumzia mti unaoitwa muembe, na tukasema unapata asili yake katika sehemu za mpaka wa India na Burma. Maelezo zaidi yanasema miembe hupatikana katika kanda nzima ya milima ya Himalaya Mashariki kwenye mpaka wa Burma na India. Kabla hatujaendelea tungependa kuwafahamisha neno la kizungu Mango lilikotoa asili yake.