Mbunge wa Malindi, Aisha Jumwa na mshikaji wake Geofrey Okuto Otieno walivamia boma la mwakilishi wa wadi ya Ganda, Reuben Katana siku moja kabla ya uchaguzi mdogo uliofanyika tarehe 17, Oktoba.
Jumwa alikiuka mila na desturi za kijamii kwa kujitosa mkutano wa wenyewe kwenye boma la watu na kuanza kuwacharaza wanaume mako? yaliyosindikizwa na cheche za matusi.