Bara la Afrika limekuwa na chanagmoto sufufu katika ulimwengu wa sasa hususan kutengwa katika maswala nyeti ya walimwengu. Mataifa ya Ulaya na mshirika wake mkuu wa Marekani wamejibandika ukuu wa wanadamu bila ya idhini ya washika dau husika. Mkuu wa tawi la chuo kikuu cha Moi mkoa wa Pwani Daktari Mbwarali Kame anaamini kwamba Afrika imenyimwa mgao wake wa haki katika sekta zote.
‘Wazungu wamewanyima wafrika haki kwa kuwagandamiza na kuwabagua katika maamuzi ya wote’ asema Kame na kuongeza kuwa Umoja wa Mataifa ni jukwaa danganyifu la kuwapandikisha wazungu na kuwashusha hadhi wafrika. Twaweza kukubaliana na maoni ya Kame kwa misingi ya matukio yanayoendelea katika ulimwengu wa sasa ya mwenye nguvu mpishe.