Kila jambo jema huwa na mwanzo mgumu tena wenye nuksi na kukorofishana ikibidi! Ingawa hivyo, mwisho wake huwa mtamu kama haluwa. Ndio hapo waambiwa cha jasho hakikosi utamu. Yaani kwa kifupi, mvumilivu hula mbivu.
Nianze kwa kusema kuwa leo hii jarida hili linaivulia kofia timu ya taifa ya soka Harambee Stars. Wanavyosema watu: twaizimia timu ya soka nchini sigareti.