Uzinduzi wa kampeni ya kusajili kupata vitambulisho maarufu kama #TokelezeaID mjini Kisumu na Katibu Mkuu wa ODM Ababu Namwamba, ni mojawapo ya mikakati itakayohakikisha kuwa muungano wa CORD unatwaa ubingwa katika kiti cha urais ifikapo 2017.
Hata hivyo utafiti na shirika la Ipsos Synovate umeonyesha kuwa ngome tatu kuu za muungano wa CORD zinavuta mkia katika usajili wa wapiga kura unaoendelea. Uzinduzi wenyewe umefanyika wakati amabapo vigogo wa muungano huo wameanza kuhakikisha wafuasi wao wamesajiliwa kupiga kura ili kushindana na wapinzani wao katika muungano wa Jubilee.