Msongamano mkubwa wa matrela ukiendelea kushuhudiwa katika Barabara Kuu ya Eldoret-Malaba viongozi wa Magharibi ya nchi sasa wanashikiza suluhu ya haraka kuafikiwa baina ya mataifa ya Kenya na Uganda kurahisisha uchukuzi.
Viongozi hao wamehusisha msongamano huo na kujikokota kwa shughuli za upimaji wa madereva hao kubaini iwapo wameambukizwa virusi vya korona au la.