The Standard Group Plc is a
multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper
print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The
Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key
influence in matters of national and international interest.
Mwanamume mmoja kwenye Kijiji cha Kubundani katika Kaunti ya Kwale ameuliwa baada ya kutuhumiwa kwamba ameathirika na Virusi vya Korona, kisa ambacho kimetokea usiku wa kuamkia leo.
Kulingana na taarifa iliyonakiliwa kwenye Kituo cha Polisi cha Diani, George Kotini Hezron ambaye alikuwa mlevi aliuliwa kilomita tatu kutoka eneo moja la burudani.
Ripoti hiyo imebainisha kwamba kotini alikutana na kundi la vijana lililoanza kumtuhumu kwamba anaugua ugonjwa wa Covid-19 baada ya ugomvi kuzuka baina yake na kundi hilo.
Baadaye, vijana hao walimshambulia kwa mawe na kumjeruhi vibaya na kufariki muda mfupi baadaye alipofikishwa katika Hospitali ya Msambweni. Kamanda wa Polisi wa Kwale Joseph Nthenge amesema msako dhidi ya waliotekeleza unyama huo unaendelezwa.
Premium Article
Get Full Access for Ksh299/Week.
Uncover the stories others won't tell. Subscribe now for exclusive access.
Stand With Bold Journalism.
Stand With The Standard.
Journalism can't be free because the truth demands investment.
At The Standard, we invest time, courage and skills to bring you accurate,
factual and impactful stories. Subscribe today and stand with us in the
pursuit of credible journalism.