NASA: Muungano sasa mahututi

Vinara wa muungano wa NASA.

National Super Alliance - NASA ndio muungano mkubwa zaidi wa upinzani kuwahi kuundwa nchini Kenya tangu uhuru ukijumuisha vyama vinne vikuu vya upinzani.

Muungano huo ulianzishwa muda mfupi kabla uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2017 kama njia ya kuimarisha makabiliano na muungano wa Jubilee uliojumuisha vyama vya URP na TNA.

Licha ya kupoteza kwenye uchaguzi mkuu, muungano wa NASA umesalia kuwa upinzani wenye nguvu na unaipa serikali wakati mgumu kwa kupiga darubini shughuli zote za serikali, iwe utoaji wa kandarasi, utekelezaji sera na utunzi wa sheria bungeni.

Kushikana mikono kwa Rais Uhuru Kenyetta na Kiongozi wa Upinzani aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga maarufu “Handisheki” kulivunja makali nguvu za muungano wa NASA baada ya vinara wengine kwenye muungano huo kunung’unika kwamba hawakuhushishwa katika mpango huo wa Handisheki.

Hata hivyo kifo cha NASA kinazidi kunukia baada ya uchaguzi mdogo wa eneo Bunge la Kibra kwani baada ya ODM, ANC na Ford Kenya kuwateua wawaniaji huku chama cha Wiper kikisalia kimya, dalili zimeanza kujitokeza bayana kwamba NASA sasa ni meli inayoelekea kuzama kabla ya kutia nanga ama kuwa? kisha wafuasi wake Mji wa Kanani kama ilivyokuwa shabaha kuu ya muungano huo ulipobuniwa.

Kampeni za kibra zilimfanya kiongozi wa ODM Raila Odinga kuwashawishi viongozi wa kisiasa kutoka eneo la Ukambani hasa kutoka Chama cha Wiper cha Kinara wa NASA, kalonzo Musyoka ili kuongeza nguvu chama cha ODM kuweza kupambana na ushindani mkali wa chama cha tawala cha Jubilee.

Mbali na mvutano kwenye kinyanganyiro cha chaguzi ndogo za hivi punde, vyama vya ANC na Ford Kenya vimekuwa vikilalamikia hatua ya ODM kutwaa hela zote za mgao wa vyama tanzu vya muungano wa NASA - Wiper, ANC na Ford Kenya.

Vyama hivyo vinadai kutopokea hata shilingi kati ya Shilingi Bilioni 4.2 zilizotolewa kwa ajili ya vyama tanzu kwenye muungano wa NASA.

Chama cha wiper kinalaumu vyama tanzu vya muungano wa Nasa kwa kile kinachoaminika kuwa sababu za kushindwa kwa Wiper na chama cha Maendeleo Chap Chap kinschoongozwa na Gavana wa Machakos Alfred Mutua kwenye uchaguzi mdogo wa wadi ya Mutonguni wiki mbili zilizopita. Mwandani wa Kalonzo aliyekuwa seneta wa Machakos Johnson Muthama ametoa matamshi ambayo yanaashiria kuvunjika kwa muungano wa NASA. Matamshi yake yanaashiria kuwepo uhusiano usio wa kuridhisha kati ya viongozi wakuu wa Muungano wa NASA ambao waliungana na kufanya kampeni ya kufa na kupona mwaka 2013 na mwaka 2017.

“Kama mwenyekiti mwenza wa muungano wa NASA anayejishughulisha na maswala ya umoja katika muungano, nataka kusema kwamba muda wangu wa kuzungmza hauja? ka, nitazungumza muda uki? ka,” alisema Muthama. Aliyekuwa Mbunge wa Kathiani Wavinya Ndeti wa chama cha Wiper alishangazwa na hatua ya Raila kumhusisha mpinzani wake wa kisiasa Gavana Alfred Mutua kwenye kikosi cha kusaka kura za ODM eneo la Kibra ilihali chama cha Maendeleo Chap Chap si miongoni mwa vyama tanzu vya muungano wa NASA.

Hii yabaini kwamba chama cha ODM kimeanza kutongoza wanasiasa wengine kwa miungano tofauti ya kisiasa na kuwaacha Musalia Mudavadi, Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula njiani ya kuelekea uchaguzi mkuu wa 2022.

Hatahivyo, kunayo mawili.

Kwanza, zile nguzo ambao azimita kutoka ukambani kweli zinao ushawishi wa kumliko Kalonzo Musyoka am ani ubepari ataka kumuonyesha Stevo aweze kubabaika.

Alfred Mutua, Kivutha Kibwana na Charity Ngilu, wote wamekuwa rangi rangile muda wao wote wa kisiasa.

Mara wamuunga mkono Kalonzo mwaka huu, mara mwaka ule wamebadilisha bao! Mama Ngilu na Kivutha Kibwana wote walipenya ugavana wa 2017 pasipo dosari baada ya makubaliano yao na kinara wa Wiper na ushirikiano wao wa ngambi ya kikamba.

Swali, ni je, wataweza kusimama kivyao pasipo ushirikiano wa ukambani kama ngome moja ya kisiasa? Washikadao wamekerwa Kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi naye ni miongoni mwa wakuu wa Muungano wa NASA waliokerwa na hatua ya Raila kuwahusisha Magavana kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Kibra.

Kwenye pita pita zake za kumpigia debe Eliud Owalo mgombea wa ANC aliyeibuka wa tatu, Mudavadi alimsuta Bwana Raila akisema hatua hiyo ilikuwa ya kinyonge sana kujihusisha na Magavana wanaotuhumiwa na kshifa za u? sadi.

“Wengi wa magavana walioitwa kuja Kibra wanavisa vya utumizi m’baya wa fedha katika kaunti zao na tayari idara ya upelelezi wa jinai na Tume ya kupambana na u? sadi EACC zinachunguza faili.”

Mudavadi amesema kwamba Magavana hao wanaji? cha nyuma ya Raila ilikupata kinga wakati wa uchunguzi. Hata hivyo chama cha ODM kupitia katibu wake mkuu Edwin Sifuna kilitoa taarifa kumkumbusha Mudavadi juu ya kuhusika katika kashfa ya Goldenberg wakati alipokuwa Waziri wa Fedha kwenye serikali ya Nusu Mkate ambapo taifa lilipopoteza mabilioni ya hela.

Muungano wa NASA umekuwa tegemeo na tumaini la wananchi hasa pale ambapo viongozi wake wanaonekana kupiga kurunzi visa vya u? sadi serikali na kila wanapoishinikiza serikali kutatua matatizo mengi ya kiuchumi na kijamii yanayowakabili raia, kuvunjika kwa NASA kunaashiria wakati mgumu kwa wananchi wanyonge nchini wanaotegemea upinzani kupigania haki zao za kimsingi.

Je muungano wa NASA unaelekea kuzikwa kabla kuingia mkondo wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2022?