Nani ampunguzia mzigo Ekuru Aukot?

Daktari Ekuru Aukot wa ‘Third Way Alliance’ 
Wahenga walinena chochote king’aracho si dhahabu na uzuri wa mkakasi kumbe ndani kipande cha mti.

Daktari Ekuru Aukot wa ‘Third Way Alliance’ amekuja na mswaada wa ‘Punguza Mzigo’ kama njia ya kurekebisha katiba ya Kenya kabla ya uchaguzi mkuu ujao wa 2022.

Hatahivyo, swali ni: Je, ni kwa nini akaja na azma hiyo wakati huu? Je, huu ni mpango wake ama kuna mabwana waliojifi cha wanaomsukuma katika jambo hili? Tukiangazia hali ya siasa nchini kwa sasa tunaona uwiano wa shaka hili kwa yanayochipuka sasa.

Ni jambo linaloeleweka kuwa sasa kuna makundi mawili pinzani walojipanga kutwaa uongozi Kenya uchaguzi ujao.

SEE ALSO :Aukot ideas to be in BBI despite fall of Punguza Mzigo

Kuna kundi linaloongozwa na Rais Uhuru na Raila al-maaruf ‘handisheki’. Kundi la pili ni lile la ‘Tangatanga; chini ya makamu wa Rais William Samoei Ruto. Akuru Aukot amekuja na mswaada wa kukarabati katiba ambao wadadisi wa kisiasa wanajikuna vichwa kwa maswali sufufu.

Huku Rais Uhuru na Raila wakipigia debe lile jopo la muungano wa kitaifa yaani “Buiding Bridges Initiative” (BBI) katka kufi kia katiba mpya , Aukot amekuja na njia m’badala ya kupinga njia hii ya vigogo wawili wa taifa.

Mdadisi wa siasa Abdulkadir Shtua asema Aukot anatumiwa na wana tangatanga kuendeleza ajenda ya kuhakikisha Ruto amejipanga kwa uchaguzi ujao na kutwaa uongozi. “Ruto na washirika wake wanaamini kuwa BBI ni kizingiti dhidi ya Naibu Rais kuwa Rais,” asema Shtua na kuongeza kuwa ‘Punguza mzigo’ ni hatua ya kuzima kasi ya BBI.

For More of This and Other Stories, Grab Your Copy of the Standard Newspaper.  

Akihojiwa na Tonny Gachoka katika kipindi cha ‘Point blank’ KTN News, Aukot alitobowa mengi ambayo yalisaliti azma yake bila mwenyewe kujua. Kwanza Aukot alishangaza wengi alipodai bila hofu kuwa ‘Raila ni muongo’ na pia si mwanademokrasia.

Tamshi hili liliwashtua wafuasi wengi wa Raila ambao wanamuheshimu na kumfuata gwiji huyu wa siasa nchini. Alipoulizwa na Gachoka kuwa haoni anaenda kinyume na Rais Uhuru kwa kupinga BBI iliyoanzishwa na yeye Uhuru kwa ushirikiano na Raila? Jibu lake ni kuwa haoni kama Uhuru anaunga mkono jopo hilo kwani hajasema kitu kuhusu jopo hilo na kuwa ni Raila anayeshindikiza BBI! Katika mahojiano hayo Aukot alitegwa na Gachoka na kuingia mtegoni.

Alipoulizwa ghafla ikiwa kuna wanawake wanaounga mkono azma yake? “Aisha Jumwa na mwakilishi wa wanawake wa Murang’a wanaunga mkono,” asema Aukot kwa haraka.

Kwa jibu lake hilo Gachoka aliuliza swali kwa watazamaji wa kipindi hicho:- “Je, Aukot ni mkweli kwa kudai Aisha Jumwa na Mwakilishi wa wanawake Murang’a wakiwa wafuasi sugu wa Ruto na wapinzani wa Raila wanaunga mkono punguza mzigo?” Sayansi ya siasa hapa ni kuwa Ruto yaelekea amebadili mbinu katika safari yake ya ikulu.Anaonyesha kutumia njia m’badala kukabili wale wanaompinga.

Anapodai kuwa Aisha Jumwa alomuasi Raila na kumkumbatia Ruto anamuunga mkono ni kuwa wamekutana naye.

Je, Akot hakupanga punguza mzigo kwa baraka za Ruto? Kupitia darubini kali ya kisiasa tunaweza kuchora hali halisi ya songombwingo na sintofahamu ya sarakasi hii ya kisiasa.

Ukweli usofi chuka ni kuwa nia ya ‘Punguza mzigo ‘ ni kuwa na Rais aliye na nguvu alivyo Rais Uhuru.

Ruto hapa nataka kurithi nafasi hiyo kwa udi na uvumba kwa jino na kucha. Jopo la BBI yaelekea kupunguza kabisa nguvu ya kiti cha Rais na kuwa na Waziri mkuu aliye na nguvu zaidi ya maamuzi. Raila yamkini anataka kiti hichi.

Aidha, BBI ina nia ya kugawanya madaraka makuu kwa kuanzisha vyeo vingine ili nchi iwe na mshikamano wa taifa.

Hapa kutakuwa na makamu wawili wa waziri mkuu. Aukot na yamkini wafadhili wake wamekuja na njia ya matamanio kwa wanawake. Punguza mzigo inataka kuwe na wawakilishi wawili tu katika ngazi ya kaunti yaani mume na mke.

“Hapa wanawake watakuwa sawa na wanaume kwa asilimia 50 kwa 50,” asema Aukot. Aukot katika azma ataka raslimali zifi kie katika ngazi ya wodi kwa wawakilishaji kwa huduma kuwa ngazi ya chini badala ya afi si ya gavana.

Kwa ujanja huu Aukot anaona mabunge ya kaunti itapitishe mswaada huu kwani ma-MCA watafaidi kifedha.

Je, ujanja huu ni njia ya kutumia maMCA kwa kuwaahidi fedha lakini kukiwa na mpango wa kuwa na Rais mmoja mwenye nguvu kule juu ambaye atakuwa Ruto? Wapinzani wa Aukot wameuliza wapi amepata fedha kupanga na kueneza falsafa ya punguza mzigo? Alipoulizwa na Gachoka kuhusu ufadhili, Aukot adai kuwa chama chake kinapata msaaada wa wananchi na sasa wamekusanya nusu milioni! Majuzi katika sherehe za utamaduni Turkana zilohudhuriwa na Ruto dhana hii ya kumuhusisha naye katika punguza mzigo zilidhiiri.

Mfuasi sugu na mpasuwa siri wa Ruto Oscar Sudi alipigia debe Punguza mzigo na kutaka watu waunge mkono. Ikumbukwe Aukot anatoka Turkana na viongozi wake wengi akiwemo gavana Nanok alidai mtu wao anaonewa.

Siku ya pili Raila alipoenda kwa tamasha hilo la Turkana gavana huyo alimshambulia akidai chama cha ODM kilimfukuza. Raila alimjibu kuwa alijifukuza mwenyewe pengine kufata asali kwengine na kuwa mlango uko wazi arudi.

Kwengineko akina Aisha Jumwa walianzisha kundi lengine la wanawake wakiijita ‘Inua Mama’ waliotupa chehe za matusi dhidi ya BBI. Kundi lengine linalounga mkono BBI pia limeanza kampeni likiwa na kina Gladys Wanga na Mishi Mboko.

Tukipima nguvu ya makundi haya pinzani tunaona kuwa upande wa BBI kuna vigogo wakuu wa siasa nchini wakioongozwa na Rais Uhuru na Raila. Wengine katika BBI ni Kalonzo Musyoka, Moses Wetangula, Musalia Mudavadi na Gideon Moi miongoni mwa wengine mbali na Atwoli kinara wa wafanyikazi aliyemshauri Ruto apunguze kasi.

Je, BBI ina nia ya kutenga nafasi kuu za waziri mkuu na manaibu kwa kina Gideon Moi, Mudavadi, Kalonzo na Raila kwa mshikamano wa taifa? Je, Aukot ni mkono wa Ruto katika mchakato mzima wa marekebisho ya katiba? Ikiwa ni hivyo, Je, kundi hili lina nguvu za kutosha za kuzima ndoto ya BBI inayoungwa mkono na kiongozi wa nchi aliye madarakani sambamba na kinara wa upinzani wakiwa na wafuasi wao walio wengi?

Do not miss out on the latest news. Join the Standard Digital Telegram channel HERE.

Get the latest summary of news in your email every morning. Subscribe below

* indicates required
Third Way AlliancePunguza MzigoEkuru Aukot