Zaidi ya maafisa mia moja wa polisi wanaohudumu katika afisi za Idara ya Upepelezi, DCI kote nchini wamefanyiwa uhamisho.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Upelelezi DCI, George Kinoti amesema maafisa mia moja ishirini na sita watatakiwa kuripoti kwenye vituo vyao vipya kufikia tarehe mosi mwezi ujao.