Rais aongoza hafla ya kukifungua kiwanda cha Rivertex Eldoret.

Rais Uhuru Kenyatta ameongoza hafla ya kukifungua tena kiwanda cha nguo cha Rivatex kilichoko mjini Eldoret. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rais amesema kwamba serikali itaendelea kuwekeza zaidi ili kuimarisha sekta ya viwanda nchini. Amesema kando na hayo, ufunguzi wa leo utakuwa wa manufaa makubwa kwani vijana wengi watapata kazi huku wakulima wa pamba pia wakinufaika, kwani watapata soko kwa zao lao.

Kuhusu kilimo cha pamba iliyobadilishwa kijenetiki yaani GMO rais ameziagiza idara zinazohusika na kilimo, afya, na elimu kuharakisha mpango wa kuanza kilimo cha pamba hiyo, inayojulikana kuwa BT Cotton.

Kwa upande wake, Naibu wa Rais William Ruto amesema serikali itaendelea na mpango wake kuhakikisha kwamba viwanda vilivyofungwa kutokana na sababu mbalimbali zinafunguliwa kwa manufaa ya Wakenya.

Ruto ametumia fursa hiyo, kusisitiza kwamba atazidi kufanya ziara kote nchini na kumuunga mkono kuhakikisha kwmba miradi ya serikali ay Jubilee inafanikiwa.

Kinyume na madai ya awali kwmaba Mbuneg wa Kaseret Oscar Sudi hataruhusiwa kuhutubu wakati wa hafla hiyo, Sundi ni miongoni mwa viongozi waliozungumza. Mbunge huyo ametoa kauli toafauti na zile za awali ambapo amesema kwamba ataendelea kumuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta pamoja za serikali yake.

Related Topics

Rivertex