Wakazi wa Koredo kwenye Kaunti ya Homa Bay, wanaishi kwa hofu kufuatia ongezeko la visa vya nyoka kuwashambulia.
Malalamiko yao yanajiri siku chache tu baada ya mwanamume mwenye umri wa makamo kushambuliwa na nyoka aina ya python akiwa shambani kabla ya wananchi kumwangamiza nyoka huyo.