Ni mbegu ya Besigye ama ni kufanana?

Mahojiano ana kwa ana na Jeff, anayefanana na Besigye

Hajatamka jina “Baba” wala hajamuona baba yake mzazi tangu kuzaliwa kake. Lakini baada ya umri wake wa sasa, Jeff Ochieng mwenye umri wa miaka 27, akajipata kafanana pakubwa na kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye. Ochieng anamwelezea Mwanahabari Kelvin Karani hali ilivyokuwa baada ya kukutana na kiongozi huyo kwa mara ya kwanza na pia jambo analotamani iwapo atakutana tena na Besigye.

Mwandishi: Hali ilikuwa vipi mlipokutana na kiongozi huyo wa Upinzani wa Uganda Kizza Besigye? Ochieng: Lilikuwa jambo la kuhangaza sana kwangu mimmi na jaama zake Kizza Besigye pi. Punde nilipofi ka Uganda nili pata umaraafu wa ghalfa ambao sikuwa nimetaraji. Mpiga picha wa kawaida kama mimi ningeliwaza kupokelewa na watu ambao sikuwajua na wengi walitaka tupige nao picha na wengi walinikumbatia hasa, wale wafuasi was chama pinzani cha FDC. Nilisubiri kama wiki jijini Kampala maana yake alikuwa amesafi ri, na pindi aliporudi niliwasiliana naye kupitia msaidizi wake na tukapanga kikao siku ya Jumapili. Jumapili ilipofi ka msadizi wake alinichukua na kunipeleka moja-kwa-moja hadi mtaa wa Kasangati kilomita 16 kutoka Kampala. Nilikuwa na uwoga nikikutana naye, lakini jamaa zake walinikaribisha kwa uzuri na kunituliza, na pindi nilipozungumza waliangua kicheko, na kufanya mzaha kua twafanana Sana na K.B . Hapo ndipo K.B aliporudi kutoka chumbani na kuni salimu kwa kutumia kiswalihi “hujambo Kijana Besigye”, siku taraji salamu hii.

Mwandishi: Kilichochangia wewe kumtafuta Kizza Besigye ni nini haswaa?

Ochieng: Mwaka wa 2006 nikiwa katika shule ya msingi ya Umoja, rafi ki yangu shuleni kasema darasani kuwa nafanana sana na Kizza Besigye, wakati huo nilikuwa simfahamu Besigye ni nani, lakini jina hilo lika baki kichwani mwangu. Sasa nilipokuwa mtu mzima nilitaka sana kujua babangu mzazi, na nilitaka mtu ambaye anaweza kunipa ukweli ili niweze kuwa na uhusiano na ukoo na tamaduni fulani, maanake yake sijaelewa na baba, ndiposa nikamfuata Besigye, kwakuwa yeye ndiye mtu ambaye twafanana sana na mama, kabla ya kuahiri dunia, hakunieleza kikamilifu kuhusu babangu. Sasa nili husishwa sana na mwanasiasa huyu na nikaonelea labda yeye ana jawabu wa uzazi wangu. Hili ndfi lolililonifanya niendee Uganda kumtafuta na kumuuliza haswa kama yeye ni babangu.

Mwandishi: Wakati mlipokutana na Kizza Besigye alikuwa na maoni gani?

Ochieng: Kwanza, hatukuzungumzia hayo, alinipa historia ndefu ya ukoo wa kabila lake la Rukiga na akanipa hidithi za mvutano baina yake na Museveni na mwishowe akanieleza ya kwamba hakuna uwezekano wa kuwa yeye ni babaangu maana yake alikuwa waziri katika serekali na hakuwahi kuishi Kenya wakati huo wa mwaka 1992 nilipozaliwa, jijini Nairobi. Alidai ya kwamba sote twatokana na Adam na Hawa, na si ajaabu watu kufanana sana lakini mimi ingwa si kwa uwazi,siku ridhishwa na matamshi hayo.

Mwandishi: Maisha yako Kenya yako vipi ikilinganishwa kuwa mnafanana na Kizza Besigye?

Ochieng: Maisha yangu si rahisi maana yake sina ajira na naishi kwa kutafuta za siku, mimi ni mpiga picha na bado hali yangu si nzuri. Wenzangu labda wako na afadhali kidogo kwa usaidizi wa wazazi wao, wazazi ambao mimi sina. Nilitaraji labda kwa kuwa tulikutana na Besigye ange nitafutia ajira ama karo za shule. Wengi wanafi kiri kuwa mimi hufaidika lakini mimi bado siko vizuri.

Mwandishi: Je marafi ki zako wanasema nini kuhusu kufanana na Kizza Besigye?

Ochieng: Wote hush-angazwa kwa vile tulikutana na Besigye na wengi bado hawajaamini. Hata nina fi kra za kubadili jina kutoka Jeff Ochieng hadi Besigye Ochieng manaake mimi na yeye ni sawa tu. Na pia hapa Kenya mara kwa mara watu huzubaa nami barabarani, isitoshe nimepata marafi ki wengi katika mtandao wa jamii kutoka Uganda name nashukuru kwa umaarufu nilionao.

Mwandishi: Labda umezungumza na Mama au watu wa familia yako kuhusu uhusiano wowote kati yako na Kizza Besigye?

Ochieng: Mama, kwa jina Grace Adhiambo, ni marahemu, na ndugu zake walikuwa wagodo na badthi ya ndugu zake mama huishi mashambani Siaya, Kenya. Mama aliaga dunia mwaka wa 2002 nikiwa na umri wa miaka 10, aliniacha katika mikono ya shangazi yangu na shangazi haku nieleza kuhusu uhusiano wangu na Besigye. Sikuweza kuzungumza na mtu yeyote kumhusu Besigye maana yake nilionelea yeye ndiye nayefanaishwa sana naye, nikaonelea labda anawezea kuwa ni yeye ndiye mzazi wangu wa kiume. Nilitaka kufi - chua ukweli mwenyewe.

Mwandishi: Tueleze kuhusu wazazi wako wa hapa Kenya?

Ochieng: Mama alinilea peke yake hadi nilipofi ka miaka 10, kisha shangazi yangu akanichukua mikononi mwake. Hakuwa na mapato vile sasa maisha hayakua rahisi nilipata tabu sana hasa katika kupata karo za shule na pia mimi sijawahi kutaja neno” baba” maishani. Shangazi pia hakuzungumzia lolote kumhusu Besigye, lakini aliniunga mkono nilipofunga safari kwenda, Uganda, akasema labda yeye ndiye.

Mwandishi: Hali imekuwa vipi tangu mara ya kwanza ulipojua kuwa mnafanana na Kizza Besigye?

Ochieng: Sikuwa na taraji tutakutana, na hata sikuwa na nia ya kujuana naye, lakini nimepata umaraafu kutokana na kufanana naye, wengi wananifahamu na nimepata kusafi ri kwenda Kampala mara mbili. Huko pia nilipata kuzungumza na watu mashuhuri, lakini hali yangu ni ileile tu sijweza ku boresha maisha yangu kwa namna yyote ile. Bado nafanya kazi ndogo ndogo ili kujikimu maishani ingawa nina matarajiio makuu. Ninahitaji usaidizi mdogo ili nitimize ndoto zangu.

Mwandishi: Je, ulikutana na familia ya Kizza Besigye?

Ochieng: La, wanawe wawili wilikuwa shuleni ng’ambo, na mkewe pia alikua ng’ambo kazini, lakini nilipata wana wa nduguye Besigye marehemu pamoja na msaidizi na wafanyikazi. Sikuwezi kuonana na familia yake haswa lakini nili karibishwa sana na nilijihisi nyumbani nikiwa kwake.

Mwandishi: Kuna mpango wowote wa kufanya uchunguzi wa DNA kati yako na Kizza Besigye?

Ochieng: Wakati nilipofanya mahojiano na gazetti la Uganda kuhusu Besigye kuwa babangu sikutaka umaarufu na nilitaka jambo hili lichukuliwe kwa makini kwa kuwa ni jambo la maana sana kwangu. Lakini wengi walilichukulia kuwa urahisi bila kuonelea kuwa hisia zangu za ndani, zita amuliwa na jawabu la Besigye kama ingetokea kuwa mimi ni mwanawe nigelipata baba kwa mara ya kwanza maishani. Wengi huniona mimi kama muigizaji tu. Swala hili ni kama mzaha kwao. Sasa nataka kuweka wazi ya kwamba naweza kutaka kufanya D.N.A ili nithibitishe kikamilifu kama Besigye ni Babangu au la, sikuwa tayari lakini nimefanya maamuzi na niko tayari, wakati huo wa awali nilikua na umri mdogo na fi kra hazikuwa zimenijia ya kuwa D.N.A itasulihisha tatizo langu. Sijui kama Besigye atakubali na sijui kama ataweza kugharamia uchunguzi huo. Nataka ukweli ujulikane na ikiwa yeye si baba yangu nita kubali. Na ikiwa yeye ni babaangu mwanzo nitamshukuru mwenyezi Mungu, pili nawezakutaka hakikisho ya kwamba mimi ni mwanawe kweli na kwa uwazi, na tatu, kwa kuwa hali yangu si nzuri nikipata urithi wa mali nitashukuru na hata akiwa babaangu nitapata uraia wa Uganda utakaoniwezesha kuishi Uganda. Akiwa babangu nitakuwa mwenye bashasha sana.

Mwandishi: Tueleze mlikutana mwaka gani na Kizza Besigye hali ilikuwa vipi?

Ochieng: Tulikutana mwezi Agosti mwaka wa 2014 mjini Kampala ambako mambo yalikuwa moto kweli. Niliambiwa swala langu na Besigye lilizungumzwa hadi bungeni na pia hapa Kenya lilizungumziwa katika vipindi mashuhuri, tokea mwaka huo jina langu la utani liwmekua Besigye, mara ya kwanza nilikua siipendi jina hili lakini nilikubali na sina tatizo nalo kwa sasa.

Mwandishi: Familia ya Kizza Besigye ambayo ulifanikiwa kukutana nayo ilitoa maoni gani?

Ochieng: Wana wa kakake walishindwa la kusema, walinitizama kila mahali hadi vidole vya miguu na kukiri kuwa mimi ni jamaa yao. Sikuweza kuelewa mazungumzo yao kwa lugha ya Kiganda, lakini niliwaacha bubumwazi, na niliwapenda niliona nikama nimepata familia mpya. Ningelitaka pia kukutana na Mamaake Anselm, mke wa Besigye pamoja na Anselm pia, lakini hiyo haikuwezekana. Lakini ni maombi yangu kama wataweza kunichukua kama mmoja wao kifamilia.

Mwandishi: Hapa Nchini unajishughulisha na kazi gani?

Ochieng: Mimi ni mpiga picha, mimi hupiga wasanii, wana mitindo na wanamziki chipukizi lakini hailipi vizuri, maana yake kufaulu huchukua muda mwingi na ninajishughulisha na shirika lisio la faida la kuwasaidia watu wenye shida za kiakilli liitwalo Yaakin Kenya, lakini ni nafasi ya kujitolea na hailipi.