Kundi la Tangatanga linahudhuria ibada Cherang'any Kaunti ya Trans Nzoia

Kundi la Tangatanga likiongozwa na Gavana wa Kiambu, Ferdinand Waititu linahudhuria ibada ambayo imeyaleta pamoja makanisa kumi na matano katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Makutano kwenye Eneo Bunge la Cherang'any Kaunti ya Trans Nzoia.

Waititu ameandamana na Mbunge wa Bahati, Kimani Ngunjiru, mwenzake wa Endebess, Daktari Robert Pukose,  Mwakilishi wa Kike kaunti, Janet Nangabo, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Kipruto arap Kirwa na aliyekuwa Mbunge wa eneo hilo, Wesley Korir.

Kwenye mkutano huo siasa zinatarajiwa kutawala ikiwamo  sakata ya dhahabu bandia na hatua ya Kinara wa Chama cha ODM, Raila Odinga kuweka wazi kwamba yeye ndiye aliyefichua sakata hiyo, mingoni mwa masuala mengine.

Ziara hiyo ya kundi hilo la tangatanga ni ya tatu kwa muda wa wiki tatu kwenye kaunti hiyo.

Do not miss out on the latest news. Join the Standard Digital Telegram channel HERE.

Get the latest summary of news in your email every morning. Subscribe below

* indicates required
kiambu governor ferdinand waititu