Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha FORD Kenya unaendelea.

Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha FORD Kenya  katika maeneo bunge yote kwenye Kaunti ya Trans Nzoia unaendelea.

Kwenye Eneo Bunge la Saboti uchaguzi huo umekamilika muda mfupi uliopita huku baadhi waliokuwa wakiwania nyadhifa mbalimbali akiwamo Elisha Khalai aliyewania nafasi ya mwenyekiti,  akielezea kutorishwa na uchaguzi huo na kwamba  majina ya baadhi ya wawaniaji yaliondolewa kwenye orodha ya wapigakura.

Hata hivyo msimamizi wa uchaguzi huo, kasisi John Okumu amesisitiza kwamba uchaguzi huo umekuwa huru na haki.

Katika uchaguzi huo,  Anthony Sikulu amechaguliwa tena kuwa mwenyekiti, Chrispinus Sinoko sasa Ni naibu wake, Enock Wangamati amechaguliwa kuwa katibu,  Milton Waswa naibu wake,  Ereza Wanjala ni mwekahazina, Fredrick Wachiye katibu mtendaji na Martin Murunga naibu wake.

Naye  Richard Hamisi akachaguliwa kuwa kiongozi wa vijana na Philis Masengeli kuwa kiongozi wa akina mama.

Related Topics

ford kenya