Naibu wa Rais William Ruto amesema yu tayari kustaafu siasani iwapo atashindwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
Aidha, Ruto amesema uongozi wa Chama cha Jubilee utajadili kuhusu atakayepeperusha bendera ya chama hicho katika kinyang'inyiro cha urais vilevile nyadhifa nyingine za kisiasa. Vilevile, amesisitiza kwamba iwapo hatateuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho, atamuunga mkono yeyote atakayeteuliwa kwani si lazima awe debeni mwaka wa 2022.