Mzozo wa kidiplomasia kati ya Kenya na Somalia huenda ukaibuka tena baada raia watatu waliokuwa na pasipoti za kidiplomasia kunyimwa kuingia nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa, JKIA jana jioni.
Kupitia mtandao wa Twitter Kituo cha Radio cha Dalsan FM nchini Somalia imewatambua watatu hao kuwa Osman Libah ambaye ni Naibu Waziri wa Maji na Kawi na maseneta Ali Hassan na Zamzam Dahir.