Serikali imetakiwa kuimarisha usalama Marsabit kufuatia mauaji ya watu 11

Viongozi wa Kaunti ya Marsabit wametoa wito kwa serikali kuimarisha usalama kwenye eneo la Forole kufuatia kisa ambapo wafugaji 11 waliuliwa siku ya Jumatatu.

Inaaminika mauaji yao yalitekelezwa na maafisa wa polisi kutoka taifa jirani la Uganda waliovuka mpaka na kuingia nchini. Inaarifiwa wakati wa kisa hicho, polisi wa akiba kwenye eneo hilo walikuwa wamepokonywa silaha zao. Hii hapa kauli ya mmoja wa viongozi hao.

Siki iliyotangulia kundi la viongozi wa Jamii ya Gabra lilisema kwamba watu waliouliwa ambao walikuwa wazee wa jamii, waliuliwa wakati walipokuwa wakihudhuria mkutano wa kuhubiri amani kati ya jamii za Kenya na Ethiopia zinazoishi mpakani pa kaunti hizo.  Chanzo cha mauaji hayo bado hakijabainika.