Katika misururu ya visa vya mauaji kwenye Kaunti ya Kakamega, bawabu mwingine ameuliwa katika eneo la Maraba usiku wa kuamkia leo huku polisi wakisema kwamba huenda ni kisa cha uhalifu wa kawaida.
Kwa upande wake, Seneta wa Kakamega Cleopas Malala ameitaka idara ya polisi kuimarisha usalama huku akitowa wito kwa vituo vya polisi kwenye kaunti hiyo kupewa vifaa vitakavyowasaidia kutekeleza majukumu yao kikamilifu.