Washukiwa 2 wa mauaji ya msichana wa umri wa miaka 20 wamekamatwa, Buruburu

Polisi wamewakamata watu wawili wanaohusishwa na mauaji ya msichana mmoja mwenye umri wa miaka 20 kwenye eneo la Buruburu, jijini Nairobi.

Washukiwa hao, Dominic Okoth na Simon Gitau walinaswa wakiwa na simu mbili zinazoaminika kuibwa kutoka kwa msichana huyo.

Katika taarifa ya Idara ya  Upelelezi, DCI msichana huyo alidungwa kisu mara kadhaa shingoni huku simu zilizopatikana zikitarajiwa kufanyiwa uchunguzi zaidi na maafisa hao.

Wawili hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya  Jumatatu kujibu mashtaka ya mauaji.

Hayo yakijiri, maafisa wa DCI wamewakamatwa wanaume wanne walionaswa katika kamera za CCTV wakimpiga mwanamume mmoja kwenye eneo ambalo idara hiyo haijalitaja.

Wanne hao wametambuliwa kuwa  Robert Momanyi,  Collins Neriko, Stanley Rimbere na Stephen Kimeu.Washukiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Jumatatu huku wengine watatu wakiendelea kusakwa.