Rias Bouteflika ajiuzulu kufutia shinikizo

 Rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika amejiuzulu wadhifa wake baada ya miaka 20 kufuatia  maandamanao ya wiki kadhaa.

Bouteflika amekuwa madarakani tangu mwaka 1999.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Shirika la Habari la nchi hiyo, kiongozi huyo tayari alikuwa ametangaza kwamba hatawania muhula wa tano kufuatia shinikizo la wananchi walioandamana katika maeneo mbalimbali.

Kadhalika Jeshi la taifa hilo lilimtaka kuondoka mapema kufuatia hali yake ya afya baada ya kuugua kiharusi miaka sita iliyopita kadhalika umri wake wa miaka 82.