Rais kuzindua usajili wa mfumo wa NEMIS Jumanne kwenye kaunti ya Machakos

Shughuli ya uzninduzi wa usajili wa mfumo wa kuwasajili watu kidijitali yaani NEMIS itazinduliwa Jumanne na Rais Uhuru Kenyatta katika Kaunti ya Machakos. Leo Gavana wa Machakos, Alfred Mutua akiandamana na maafisa wa usalama wa Kaunti ya Machakos pamoja na wengine wa Ikulu wanatarajiwa kuzuru eneo la Mwala kaunti hiyo ambapo hafla hiyo itafanyika.

Rais Uhuru Kenyatta atazindua mfumo huo hapo kesho kutegemea na uamuzi ambao mahakama itatoa leo kufuatia kesi ambayo imewasilishwa na Tume ya Kutetea Haki za binadamu KHRC, Nubian Rights Forum na Kenya National Commission on Human Rights KNCR ikipinga kuzinduliwa kwa mfumo huo.

Makundi hayo matatu yanadai kuwa huduma namba haifai kutumika kumnyima Mkenya haki ya kupata huduma muhimu kulingana na katiba na kuwa watu wa asili ya Kisomali na wengine wa Nubia watatengwa.

Kufikia sasa, Manaibu wa Chifu wa kaunti zote 47 wametayarishwa kuanza usajili huo utakaotumia siku 45.

Mpango huo ulifanyiwa majaribio kwenye kaunti kumi na tano ambazo ni Nairobi, Uasin Gishu, Kisii, Kajiado, Baringo, Marsabit, Wajir, Nyandarua miongoni mwa nyingine.

SEE ALSO :Uhuru’s trip to Jamaica rekindles memorable ties

Usajili huo unalenga kupata sajili moja, ambapo kila mtu atapewa nambari maalumu kwa jina Huduma Namba na hakuna atakayehudumiwa na serikali bila kuwa na nambari hiyo maalumu.

Baadhi ya data zitakazochukuliwa ni picha ya kila anayesajiliwa, jina, jinsia, tarehe ya kuzaliwa, umri, eneo la kuzaliwa, uraia, maelezo kuwahusu wazazi, nambari za simu, anwani ya baruapepe, anwani ya mahali anakoishi na hali ya ndoa. Shughuli hii itagharimu kati ya shilingi bilioni 5 na shilingi bilioni 6.

Naibu Kamishana wa Jomvu kwenye Kaunti ya Mombasa, Paul Kinyanjui amewashauri wakazi kutoamini madai kwamba watatolewa chemechembe ya damu DNA kwenye shughuli ya usajili wa mfumo mpya wa kidigitaji NIIMIS Huduma namba

For More of This and Other Stories, Grab Your Copy of the Standard Newspaper.

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.

uhuru kenyatta