Afisa wa kitengo cha Flying Squad ameuliwa usiku wa kuamkia leo na washukiwa wa uhalifu mjini Taveta kwenye Kaunti ya Taita Taveta.
Afisa huyo alikuwa na wenzake wakati alipopigwa risasi na watu wawili ambao vilevile wamehusishwa na uhalifu uliotekelezwa mjini Mombasa na kunaswa katika kamera za CCTV.