Kakaye Mishi Mboko atarajiwa kuzikwa leo

Daktari anayesemakana kujiua akiwa mafunzoni nchini Cuba Dkt Hamisi Ali atazikwa leo. Ali ambaye ni kakaye mbunge wa Likoni, Mishi Mboko atazikwa katika eneo la Shika Adabu eneo hilo la Likoni

Mazishi haya yatajiri wakati kifo chake kimesababisha kuangaziwa upya kwa maslahi ya madaktari takribana 50 waliotumwa kwa mafunzo nchini humo.

Serikali sasa  imeahidi kuwa itawalipa marupurupu zaidi madakatri hao 50. Katibu wa Wizara ya Afya Susan Mochache amesema madktari hao sasa watakuwa wakilipwa shilingi elfu mia moja arubaini na nne kila mwezi kinyume na shilingi elfu hamsini mia nane ambazo wamekuwa wakilipwa. Hatua hii inamaanisha kuwa kila daktari atalipwa shilingi laki nne kila mwezi, pamoja na mshahara ambao walikuwa wakilipwa nchini kabla ya kuelekea Cuba.

Mochache amesema pesa hizo zitaanza kulipwa kuanzia mwezi ujao. Wakati huo huo amesema madaktari hao hamsini akiwamo Daktari Ali Juma ambaye alijiua Jumapili iliyopita wamelipwa jumla ya shilingi milioni 13.4 huku akisema serikali imetenga shilingi milioni mia tatu kwa mpango huo.

Mochache ambaye alihojiwa na kamati ya Bunge ya Afya alitakiwa kuelezea mazingira ya kazi ya madaktari hao kufuatia ripoti kwamba ni magumu hali iliyosababisha mmoja wao kujiua. Hata hivyo amekana taarifa kuwa madaktari hao wananyanyaswa akisema serikali inawashughulikia ipasavyo.

Amesema kwa sasa wanasubiri ripoti ya upasuaji uliofanyiwa mwili wa marehemu kabla ya kutoa taarifa kamili kuhusu kilichosababisha kifo chake. Tayari kundi la wataalam likiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara Rashid Iman limeelekea Cuba, kutathimini hali na linatarajiwa kurejea nchini baada ya siku tano.

Related Topics