Matiang'i awahakikishia wakazi wa Lamu huduma bora

Waziri wa Masuala ya Ndani ya Taifa Daktari Fred Matiang'i, amesema  serikali kamwe haita wavumilia maafisa wazembe kuhudumu katika vitengo mbalimbali huku wananchi wakitaabika kutokana na utendakazi duni.

Kwenye kikao na wakazi wa Lamu mapema leo, waziri Matiang'i  amesema ni wajibu wa viongozi wa Serikali kutelezaji  majukumu  yao kwa mujibu wa sheria huku akisisitiza umuhimu wa ushiriano baina ya maafisa wa serikali.

Akiandamana na Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma DPP Nordin Haji, Matiang'i amewaamurisha maafisa wa usalama kuwanasa na kuwashtaki washukiwa wa visa vya ubakaji huku ikibainika kwamba eneo la Lamu limeshuhudia visa vyingi vya dhuluma za kingono dhidi ya watoto.

Wakati uo huo,  Waziri ameahidi kuwekwa mikakati kabambe ya kutatua mizozo ya Ardhi, akisema kwa ushirikiano na waziri wa Ardhi Farida Karoney, serikali inakwenda kutafuta suluhu ya kudumu kupitia utoaji wa hati miliki za mashamba.

Aidha amewahakikishia wavuvi wa Lamu kuwa serikali itawasajili kupitia njia ya elektroni ili kuwapeushia mahangaiko ya kujisajili kila siku kabla ya kuruhusiwa kwenda kuvua baharini.

 

Related Topics