Nanok awahamisha mawaziri 4

Gavana wa Kaunti ya Turkana, Josephat Nanok amefanya mabadiliko katika Baraza lake la Mawaziri huku mawaziri wanne wakiathirika. Jennifer Nawoi ambaye alikuwa Waziri wa Utalii, Utamaduni na Mali Asili amehamishwa katika Wizara ya Biashara , Jinsia na Vijana huku nafasi yake ikichukuliwa na Charles Ewoi Lokiyoto  ambaye awali alikuwa katika Wizara ya Usiamamizi wa Umma na Masuala ya Dharura.

Esther Lokiyo Lokwee  vileviel ameondolewa katika Wizara ya Ardhi na Miundo Msingi hadi wizara hiyo ya usimamizi wa umma na masuala ya dharura.

Wa mwisho kuhamishwa ni Anthony Apalia ambaye ametoka ametoka Wizara ya Biashara hadi Wizara ya Ardhi na Miundo Msingi. Kwa mujibu wa Nanok, mabadiliko haya yanalenga kuboresha utoaji huduma.

Wote waliohamishwa wametakiwa kuanza kazi katika nyadhfa zao mpya chini ya kipindi cha saa 72.

SEE ALSO :Pensioners turn to Kenya's DCI in new bid to recover Sh1.2b assets

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.