Walemavu wa ngozi walalamikia kutengwa Taita Taveta kutokana na dhana potovu

Suala la watu wenye ulemavu wa ngozi kutengwa kwa dhana kuwa ni laana katika jamii kwenye Kaunti ya Taita Taveta linafaa kukomeshwa.

Muungano wa watu wenye ulemavu kwenye kaunti hiyo unasema kuwa watu hao wanatengwa hivyo n sharti wakazi wafahamu kuwa ni hali tu ya maumbile tu, hivyo jamii inapaswa kuwakumbatia wenye ulemavu na kuwasaidia kwa kila hali.

Aidha wanasema kuwa ipo haja ya serikali ya kaunti hiyo kuwasambazia mafuta maalum wanayotumia ili kujikinga dhidi ya miale ya jua.

For the latest news in entertainment check out Sde.co.ke and Pulser.co.ke , for everything sports visit Gameyetu.co.ke and ladies we have you covered on Evewoman

Walemvu Ngozi Taita Taveta