Moto umeteketeza zaidi ya ekari 150 katika msitu wa Maasai Mau kwenye mkasa wa kuanzia Jumatatu wiki hii

Moto umeteketeza zaidi ya ekari 150 katika msitu wa Maasai Mau kwenye mkasa wa kuanzia Jumatatu wiki hii. Inaarifiwa wakazi wanaoishi karibu na msitu huo wamelazimika kuhama baada ya moto huo kuteketeza baadhi ya nyumba zao.

Mwenyekiti wa Idara ya Misitu kwenye Kaunti ya Narok, Mwai Muraguri amesema moto huo ulianzia katika eneo la Olposimoru na kusambaa hadi maeneo la Olenguruone huku wanyamapori wakiathirika zaidi.

Muraguri aidha amesema ndovu zaidi ya 40 na mamia ya nyati wako kwenye hatari ya kufa kufuatia moto huo ambao chanzo chake hakijabainika. Juhudi za kuuzima moto huo zinaendelea.

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.

Moto Msitu Mau