Polisi wapata bastola aina ya Bereta na risasi kumi na tano nyumbani kwake Rashid Echesa

Polisi waliovamia nyumba ya aliyekuwa Waziri wa Michezo Rashid Echesa mtaani Karen, Nairobi walipata bastola aina ya Bereta na risasi kumi na tano.

Kwa mujibu wa ripoti iliyorekodiwa katika Kituo cha Polisi cha Kilimani, polisi wanachunguza iwapo Echesa ambaye alifutwa kazi na Rais Uhuru Kenyatta tarehe mosi mwezi huu, ana leseni halali ya kumiliki bastola hiyo.

Waziri huyo wa zamani amethibitisha kutekelezwa kwa msako huo nyumbani kwake akisema kuwa aliwasilisha leseni ya umiliki wa silaha kwa maafisa hao.

For the latest news in entertainment check out Sde.co.ke and Pulser.co.ke , for everything sports visit Gameyetu.co.ke and ladies we have you covered on Evewoman

rashid echesa