Daktari Mkenya Kakaye Mbunge wa Likoni Mishi Mboko afariki Nchini Cuba akihudhuria masomo

Serikali imethibitisha kifo cha daktari Mkenya mwenye umri wa miaka 50 ambaye alisafiri kwenye taifa la Cuba kuhudhuria masomo  katika mpango wa ushirikiano baina ya Kenya na  Cuba

Katika taarifa rasmi,  Wizara ya Afya imesema Dkt Hamisi Ali Juma aliaga dunia Jumapili Tarehe 17 mwezi huu na bado haijabainika ni nini kilisababisha kifo chake.

Dkt Ali Juma alikuwa miongoni mwa madaktari 50 ambao walikuwa wametumwa na serikali ya kitaifa kupata mafunzo zaidi  katika makubaliano baina ya  mataifa hayo mawili.

Hata hivyo Wizara ya Afya imesema mipango wa kusafirisha mwili wa Daktari huyo kutoka Taifa la Cuba umeanzishwa na Balozi wa Kenya kwa ushirikiano na Serikali ya Cuba.

Dadaye mwendazake amabye ni Mbunge wa Likoni Mishi Mboko amemuomboleza kakaye na kusema kuwa chanzo cha kifo chake bado hakijatambulika huku upasuaji ukitarajiwa kufanyika leo.

Related Topics