Je, Ndege aina ya 737 8 Max iliyoanguka ilikuwa na hitilafu?

Huku familia za watu 157 walioaga dunia wakisubiri kufunga ukurasa wa maombolezo kwa njia mbalimbali hofu waliyokuwa nayo wengi kuhusu kilichosababisha ajali hiyo ya ndege kimethibitishwa kufuatia vidokezo vya awali vya uchunguzi wa kifaa cha kunakili data za ndege kwa kiingereza Blackbox.

Kwa mujibu wa taarifa ya mmoja wa wachunguzi kuna mfanano mkubwa baina ya jinsi ajali hiyo ilivyotokea  na ile iliyohusisha ndege sawa na hiyo ya 737-8-Max  mwaka uliopita nchini Indonesia.

Taarifa hizi za awali ni kutokana na vifaa viwili  vya blackbox- kimoja cha kunakili data na kingine cha kunakili sauti katika eneo la kuendeshea ndege yaani Cockpit. Taarifa hizo zinaeleza wazi kwamba katika ajali zote mbili- Ethiopia Airines na Lion Air, ndege zilianguka muda mchache baada ya kupaa angani yaani dakika sita na 13 mtawalia.

Kadhalika katika ajali zote mbili marubani waliomba kurejea katika uwanja wa ndege baada ya ndege kuanza kuyumbayumba na hatimaye kushika mwendo wa kasi ikielekea chini.

SEE ALSO :Before you support or opt for cremation, think twice

Kufuatia uchunguzi uliofanywa baada ya ajali ya Lion Air libainika kwamba ndege hiyo aina ya 737 8 Max ilikuwa imezua wasiwasi katika safari zake za awali licha ya kuwa mpya kabisa na kubainika ilikuwa na dosari katika mtambo wake  wa Maneuvering Characteristics Augmentation System MCAS, mtambo ambao unafanya ndege kulenga chini kwa kasi inapopata hitilafu ambazo zinaweza kufanya ianguke kwa lugha ya kitaalamu ' Stalling'. Hatua hiyo inatokana na taarifa inazopokea kutoka vifaa vinavyojulikana kama 'sensors'.

Kifaa hicho kiliwekwa baada ya muundo  wa Boeing kubadilishwa na injini kusongezwa sehemu za mbele jambo lililofanya ndege kulenga juu ndiposa kifaa kikawekwa ili kuirejesha na kulenga  chini bila kumfahamisha rubani. Hata hivyo ndege hiyo ina kifaa ambacho kinaweza kuzima  mtambo huo japo marubani hawakufahamishwa kukihusu.

Nchini Ethiopia uchunguzi unaelekea huko huko kwa teknolojia ambayo imemfanya rubani kuwa zuzu katika baadhi ya matukio. Hata hivyo  uchunguzi zaidi  unapofanywa kutoka kwa mitamb ili kubainisha  zaidi swali ambalo wengi huenda wakajiuliza ni Je? mbona  ndege nyingine 371 za aina ya 738 8 Max zimekuwa zikipaa na kutua kote duniani pasi na ajali ? Ukweli  ni kuwa sula la changamoto katika teknolojia ya ndege lilikuwa limebuliwa mara si moja na marubani kote duniani.

For More of This and Other Stories, Grab Your Copy of the Standard Newspaper.

Katika ripoti ya Shirika la Masuala ya Angani, Marekani NASA, mmoja wa marubani analalamikia vikali kutojumisuihwa kwa mtambo huo wa MCAS katika vitabu vya maelezo ya jinsi ya kutumia ndege hiyo yaani Flight Manual

Hii si mara ya kwanza kwa hofu kuhusu muundo wa ndege aina aina za  Boeing kuibuliwa. Mwaka 2014 Shirika la Habari la Alajzeera liliangazia jinsi utaratibu wa kiusalama ulikiukwa katika kuunda ndege aina ya Boeing 787.

SEE ALSO :CBC will exacerbate economic inequality and burden parents

Baadhi ya hatua zilitajwa kuharakishwa  kwa shughuli yenyewe na wafanyakazi waliolalamika kufutwa. Hata hivyo la kushangaza  zaidi ni kwamba baadhi ya wafanyakazi walipa kutopanda ndege ambayo wenyewe waliunda. Hofu  hii ilithibitishwa na  visa kadhaa vya ndge kuvuja mafuta ama mfumo wa umeme kusababisha moto kutokanana batari iliyokuwa ikitumika. Hata  hivyo visa vingi vilikabailiwa na kusuluhishwa.

Hata hivyo Shirika la Boeing halijafungia masikio masuala haya yote. Katika taarifa ya hivi punde zaidi chini ya kipindi cha wiki mbili kampuni hiyo itatokea tole la hivi punde zaidi za mtambo huo kadhalika kutoa mafunzo kwa marubani kuhusu mfumo huo mpya. Ni matumaini kwamba hili pengine hili huenda likarejesha ndege 371 za Boeing angani zikiwa salama.

Do not miss out on the latest news. Join the Standard Digital Telegram channel HERE.