Polisi walaumiwa kufuatia kifo cha mwanafunzi wa UoN

Na Mike Nyagwoka,

NAIROBI, KENYA, Polisi wanaendelea kulaumiwa kufuatia kifo cha aliyekuwa Kiongozi wa Wanafunzi Chuo Kikuu cha Nairobi Samuel Ragira.

Wanatuhumiwa kwa kumfyatulia risasi Ragira jana katika eneo la Klabu katika chuo hicho alipokuwa akilalamikia njama ya watu fulani kunyakua vibanda vya kibiashara katika eneo hilo.

Aidha, wanadai kwamba kifo chake kilisababishwa na utepetevu wa maafisa wa polisi kwa kutoruhusu Ragira kupata matibabu ya dharura na kusababisha kifo chake akikimbizwa hospitalini.

Inaarifiwa mzozo uliibuka kufuatia usimamizi wa maduka yaliyo chuoni humo baina ya wanafunzi walio chuoni humo na wale wa zamani katika eneo linalojulikana sasa kama Klabu na ambapo inaarifiwa ndiko akikofyatuliwa risasi. 

Related Topics

UoN