Rais Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Somalia Mohamed Farmaajo ,wamefanya mazungumzo kuhusu mzozo wa kunadiwa kwa maeneo ya bahari yaliyo mkapani pa Kenya na Somalia. Mkutano huo umeongozwa na Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed hapa jijini Nairobi.
Kwenye ujumbe wake katika mtandao wa kijamii wa twiter baada ya mazungumzo hayo, Abiy amesema mataifa haya mawili yameafikiana kushughulikia mzozo wa kidiplomasia .Ahmed Aby amesema wawili hao wanatarajiwa kuendeleza mazungumzo muhimu ili kukuza umoja wa kieneo ,amani,usalama na maendeleo. Juma lililopita Abiy, aliongoza mikutano miwili tofauti ya kidiplomasia na Kenyatta na Farmaajo.