Waziri mpya wa Michezo, Tamaduni na Turathi Balozi Amina Mohammed asubuhi hii amechukua rasmi wadhifa huo kutoka kwa mtangulizi wake Rashid Echesa. Hafla ya kumkabidhi mamlaka imefanyika katika makao makuu ya wizara hiyo kwenye jumba la Kencom, mjini Nairobi.
Ikumbukwe Echesa alisimamishwa kazi na Rais Uhuru Kenyatta wakati alipofanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri Ijumaa wiki iliyopita. George Magoha alichaguliwa kuchukua nafasi ya waziri Amina kwenye Wizara ya Michezo.