Mwajiri wa Naibu Jaji Mkuu akamatwa

Maafisa wa polisi wamemtia mbaroni mwajiri wa Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu Cosmas Mutua , kufuatia madai ya mwaka jana kuwa alitekwa nyara na watu watatu. Mutua alidai kuwa watu waliomteka nyara walitaka kujua anakoishi Naibu Jaji.

Mkurugenzi wa Idara ya upelelezi DCI, George Kinoti anasema Mutua hakutekwa nyara jinsi anavyodai kwenye taarifa aliyowasilisha katika kituo cha polisi cha Kilimani Novemba 8 mwaka uliopita.

Ikumbukwe Mutua aliambia polisi kwamba alitekwa nyara katika barabara ya Ngong alipokuwa amekwenda kununua bidhaa zake katika duka Kuu la Nakumatt Junction.

Aidha mwezi Oktoba mwaka jana mlinzi wa Mwilu alipigwa risasi na kujeruhiwa na watu wasiojulikana ambao pia walitoweka na bunduki yake.

Ikumbukwe Mwilu anakabiliwa na tuhuma za ufisadi kukiwamo kukwepa kulipa kodi, matumizi mabaya ya ofisi na kupokea hongo. Hata hivyo aliwasilisha kesi mahakamani dhidi ya serikali akilenga kusitisha kesi ya ufisadi dhidi yake. Kesi hizo mbili zingali zinaendelea.

Related Topics

Mwilu Jaji