Jane Kiano ametajwa kuwa mmoja wanawake waluopigani haki bila uoga

Serikali itatenga siku ya kuwakumbuka na kuwatambua wanawake ambao wamechangia kuafikiwa kwa mabadiliko humu nchini.

Akihutubu wakati wa ibada ya wafu ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Maendeleo ya Wanawake, Jane Kiano katika Kanisa la St. Francis ACK eneo la Karen, Rais Uhuru Kenyatta hata hivyo amesema kuwa ni vyema kuwatambua wanawake hao wakiwa wangali hai.

Pendekezo hilo lilitolewa na Kinara wa ODM, Raila Odinga ambaye amesema Kenya linastahili kuwakumbuka wanawake wote waliochangia uhuru na usawa nchini.

Mwendazake Kiano ametajwa kuwa mmoja wa wanawake waliopigania haki za wanawake bila uoga.

Kiano alifariki dunia Alhamisi wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka sabini na minne baada ya kuugua saratani ya mapafu kwa muda mrefu. Ikumbukwe alikuwa mmoja wa waasisi wa Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa, NCIC.

Jane alikuwa mkewe marehemu, Julius Gikonyo Kiano, aliyekuwa Waziri, mzalendo na Mkenya wa kwanza kusomewa shahada ya PHD.