Na Mate Tongola
Maafisa wa Idara ya Uplelezi, DIC kwa sasa wanaendelea kumhoji Gavana wa Migori, Okoth Obado kufuatia kisa cha kuuliwa kwa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Rongo, Sharon Otieno.
Hii ni mara ya pili kuhojiwa kwa Gavana huyo ambaye ametajwa pakubwa na mauaji hayo. Kuhojiwa kwake leo hii kunajiri baada ya uchunguzi wa VINASABA yaani DNA kubainisha kuwa ujauzito wa marehemu Sharon ulikuwa wake.
Ikumbukwe msaidizi wa Gavana Obado, Michael Oyamo na aliyekuwa Mwakilishi Wadi wa Kanyadoto, Lawrence Mula ni miongoni mwa washukiwa wa mauaji hayo ambao wanaendelea kuzuiliwa.
Fact‑first reporting that puts you at the heart of the newsroom. Subscribe for full access.
- Unlimited access to all premium content
- Uninterrupted ad-free browsing experience
- Mobile-optimized reading experience
- Weekly Newsletters
- MPesa, Airtel Money and Cards accepted