×
App Icon
The Standard e-Paper
Kenya's Bold Newspaper
★★★★ - on Play Store
Download Now

Uhuru na Ruto waapishwa

Beatrice Maganga
Uhuru na Ruto waapishwa
Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake, William Ruto  wameapishwa rasmi kuchukua hatamu za uongozi kwa muhula wa pili huku Rais akitangaza kuwa na ajenda mbili kuu miongoni mwa ajenda zake kwa taifa. Suala la kuwaunganisha Wakenya ni mojawapo wa ajenda hizo huu ikizingatiwa migawanyiko ambayo imeshuhudiwa nchini kwa kipindi kirefu cha uchaguzi.
Ajenda nyingine kuu ya Rais ni kuhakikisha kwamba Wakenya takriban milioni 13 wanasajiliwa katika mpango wa Bima ya Kitaifa ya Afya, NHIF kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake. Akitangaza kukamilika kwa kipindi cha uchaguzi kufuatia kuapishwa kwake, Rais amesema analenga kujumuisha ajenda mbalimbali za wapinzani wake, kwa manufaa ya Wakenya.
Wakati uo huo Rais ameahidi kuchukua hatua kali dhidi ya maafisa wa umma wanaozembea kazini na kutatiza harakati za kutimiza ahadi zake kwa wananchi, vilevile kuishauri idara ya mahakama kutokubali kutumiwa kutatiza utendakazi wa serikali kupitia kesi mbalimbali. Aidha amesema bunge litatumiwa kupitasha sheria dhidi ya matumizi mabaya ya raslimali za umma ili kuhakikisha fedha za mlipa kodi zinatumiwa vilivyo.
Rais Kenyatta amesema kipindi cha uchaguzi kiliziyumbisha idara mbalimbali za serikali japo kipindi hicho kilitoa fusa kwa kila idara kudhihirisha utendakazi wake huku akisema Mahakama ya Juu ilidumisha uhuru wake katika kufanya uamuzi kwa mara ya pili kuhusu kesi ya kupinga ushindi wake na kuipongeza Tume ya Uchaguzi, IEBC kwa kujibidiisha licha ya kukabiliwa na kibarua kigumu cha kuandaa uchaguzi.
Si hayo tu, ameisifu serikali yake kwa kutekeleza mengi katika hatamu ya kwanza ya uongozi kukiwamo kuboresha huduma za umeme, uzinduzi wa reli ya kisasa, SGR, kufanikisha ugatuzi, kuzibwa kwa mianya ya udanganyifu katika mitihani ya kitaifa na sasa kuagiza kwamba watahiniwa wote waliofanya KCPE mwaka huu wajulishwe shule walizochaguliwa kujiunga nazo kabla ya Krismasi.
Katika juhudi za kuimarisha uhusiano baina ya Kenya na mataifa mengine ya Afrika, Rais ameagiza kuondolewa kwa vizingiti vya usafiri na kufanya biashara kwa raia wa mataifa ya Afrika Mashariki wanaolizuru taifa hili vilevile kukabidhiwa viza mara moja kwa raia wengine wa mataifa ya Afrika wanaotaka kuja Kenya.
Ahadi nyingine za Rais ni kubuniwa kwa nafasi zaidi za kazi, wananchi kupata makazi bora ya kuishi, kupunguzwa kwa gharama ya umeme kwa kampuni za utengenezaji wa bidhaa mbalimbali kuanzia Disemba Mosi, kumairishwa kwa sekta ya kilimo nakadhalika.
Na huku Rais akimfisu mkewe, Bi. Margaret Kenyatta kwa kumuunga mkono katika harakati za uongozi vilevile naibu wake William Ruto kwa kufanikisha uongozi wao, Ruto kwa upande wake ameahidi  kushirikiana na Rais katika kuafikia umoja wa wananchi. Ruto amesema wakati umewadia wa Wakenya kuepuka kugawanywa kwa misingi ya kikabila.
Get Full Access for Ksh299/Week
Unlock the Full Story — Join Thousands of Informed Kenyans Today
  • Unlimited access to all premium content
  • Uninterrupted ad-free browsing experience
  • Mobile-optimized reading experience
  • Weekly Newsletters
  • MPesa, Airtel Money and Cards accepted
Already a subscriber? Log in

Related Topics