Please enable JavaScript to view advertisements.
×
App Icon
The Standard e-Paper
Home To Bold Columnists
★★★★ - on Play Store
Download App

Magari ya kubeba abiria yapigwa marufuku kuingia katikati ya jiji

Magari ya kubeba abiria yapigwa marufuku kuingia katikati ya jiji

Carren Omae
Katika hatua ya kupunguza msongamano katikati ya jiji la Nairobi, serikali ya kaunti imeyapiga marufuku magari ya uchukuzi wa umma dhidi ya kuingia ndani ya jiji. Katika taarifa rasmi iliyochapishwa katika gazeti rasmi la serikali na ambayo ilitiwa saini na Kaimu Katibu wa Kaunti Leboo ole Morintant, serikali ya kaunti hii aidha imeondoa idhini waliyokuwa wamepewa wahudumu wa magari hayo huwashusha au kuwabeba abiria katikati ya jiji. Morintent amesema watashirikiana na maafisa wa polisi na wale wa Mamlaka ya Usalama Barabarani, NTSA kufanikisha mpango huo, unaotarajiwa kuanza rasmi Jumatano ijayo.
Katika mpangilio huo, mpya magari yanayoingia katikati ya jiji kutoka Barabara Kuu za Waiyaki na Uhuru na Barabara ya Kipande yameshauriwa kuwashukisha abira katika kituo cha Fig Tree Terminus A. Aidha magari yanayoingia kutoka Barara Kuu ya Thika, Barabara ya Kiambu na Murang'a, wameshauriwa vilevile kuwaacha abiria katika kituo hicho, terminus B.
Aidha magari yanayotoka Kenol, Nyeri na Meru na magari yanayotoka nje ya Nairobi kupitia Barabara Kuu ya Uhuru yameshauriwa kuwaacha abiria wa kituo cha Park Road. Vilevile magari kutoka Barabara za Mombasa na Lang'ata yatakuwa yakiegeshwa katika kituo cha Hakati. Yale kutoka Ngong yataegeshwa katika kituo cha mabasi cha  Railways huku yanayotoka barabara za Jogoo na Lusaka yakitarajiwa kuwabeba na kuwashusha abiria katika kituo cha mabasi ya Muthurwa.
Katika agizo hilo mpya magari yote ya kubebea mizigo na abiria kutoka nje ya Nairobi yameshauriwa kutumia kituo cha mabasi cha Country Bus.
Ikumbukwe wafanyabiashara hasa wanaomiliki maduka katikati ya jiji wamekuwa wakilalamikia msongamano mkubwa wa watu unaosababishwa na idadi kubwa ya magari yanayoingia jijini, hivyo kuathiri biashara zao.?

Premium Article

Get Full Access for Ksh299/Week.

Bold Reporting Takes Time, Courage and Investment. Stand With Us.
Continue Reading  →
What you get
  • Unlimited access to all premium content
  • Ad-free browsing experience
  • Mobile-optimised reading
  • Weekly newsletters & digests
Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payments Kenya's most trusted newsroom since 1902
Support Independent Journalism

Stand With Bold Journalism.
Stand With The Standard.

Journalism can't be free because the truth demands investment. At The Standard, we invest time, courage and skills to bring you accurate, factual and impactful stories. Subscribe today and stand with us in the pursuit of credible journalism.

Pay via
M - PESA
VISA
Airtel Money
Secure Payment Kenya's most trusted newsroom since 1902

Related Topics