Washukiwa wa ufisadi Kilifi wakosa kufika mahakamani

Na Kelvin Karani

Washukiwa wanne ambao ni wafanyakazi wa Kaunti ya Kilifi na ambao nosari zao passwords zilitumika katika wizi wa shilingi milioni 51 kupitia mfumo wa IFMIS wamekosa kufika mahakamani.

Washukiwa Jacob Kazungu Khonde, Johnson Nyamawi Gabo,Timothy Malingi Koe, Paul Teido Mwazo,John Kahindi Kalume ,Dickson Mwangone Kalume ,Lenox Mwadzoya Mwasirya, Josephine Felix Muramba na Daniel Baha Nguma walikosa kufika mahamani mapema leo kujibu mashtaka ya wizi dhidi yao.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kilifi Leah Wasige, wakili wa washukiwa Nyongesa Duncan ameambia mahakama kuwa wateja wake wamekosa kufika mahakamani kwani walikuwa wanatoa taarifa zaidi za wizi huo kwenye ofisi za Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadfi EACC mjini Mombasa.

Washukiwa hao ambao walikuwa wafanyakazi wa Kaunti ya Kilifi waliachishwa kazi baada ya wizi wa fedha hizo kugundulika, huku Gavana Kingi akisema wachunguzwe.

Hata hivyo wakurugenzi watatu wa baadhi ya kampuni zilizotajwa kuhusishwa na wizi huo tayari wameshtakiwa katika mahakama hiyo ya Kilifi.

Kesi dhidi ya wafanyakazi hao itatajwa Desemba 13 ili washukiwa washtakiwe rasmi.

Related Topics

EACC Kingi