Mwezi mmoja baada ya bomoa bomoa iliyowaacha wengi bila makao katika mitaa ya syokimau, kijiji cha mitumba, kiang;ombe na maasai, waathiriwa wengi wa ubomoaji huo wangali wanakabiliana na harasa iliyowakumba. Wengi wangali wanaishi na jamaa na marafiki waliowakaribisha, na wengine, wameshindwa kuanza upya maisha yao, wanasema hawajui waanze vipi.