Kuna shaka kuu kwamba ushauri na mawaidha yanayotolewa kwa wakenya kote nchini kupitia mitandao, stesheni za redio na simu za rununu huenda haitatui shida au matatizo yanayowazonga raia hususan matatizo ya kuzongwa na fikra.Hadi sasa wakenya wengi hutazamia aidha kupata mawaidha kupitia vipindi tofauti au ujumbe wa simu za rununu au kwa marafiki badala ya kuwasiliana na wataalam katika taaluma ya ushauri kwa kimombo counselling. Je nia kuu ya mbinu hizi mpya za ushauri ni biashara au kuwasaidia walio na matatizo?