KRA yanasa magari yaliyoingizwa humu nchini bila kulipiwa kodi

Na Mike Nyagwoka

Halmashauri ya Ukusanyaji Kodi Nchni, KRA inaendeleza uchunguzi dhidi ya magari matano yaliyonaswa katika Barabara ya Mombasa jana. Magari hayo, matatu aina ya Rangerover, moja aina ya Landcruiser V8 na moja aina ya Subaru yanaaminika kuingizwa nchini bila kulipiwa ushuru.
Magari hayo ni miongoni mwa 300 ambayo yamenaswa nchini mwaka huu kwa kuingizwa nchini bila kufuatwa kwa utaratibu uliowekwa.
Mapema mwezi huu, magari mawili yalinaswa katika kontena moja katika Bandari ya Mombasa yakiingizwa nchini kisiri huku ikibainika kwamba kontena hilo lilikuwa limesajiliwa kuwa lililobeba baiskeli. KRA imesema itaendelea kuimarisha doria dhidi ya biashara haramu ya kuingiza magari nchini bila kulipiwa ushuru.

 

Related Topics

KRA Mombasa