Katibu Mkuu wa Chama cha UDA, Veronica Maina amesisitiza kwamba Kenya Kwanza itafanya mkutano wake tarehe 6 Agosti katika Uwanja wa Michezo wa Nyayo, akipinga kupokonywa leseni ya kuendesha mkutano siku hiyo. Kwa mujibu wa Maina, tayari Kenya Kwanza imelipia uwanja huo na hawatakubali kubatilishwa.
Ijumaa wiki hii Kamati ya Kampeni za Ruto iliwasilisha kesi mahakamani kupinga hatua ya Idara ya Michezo kusema kwamba uwanja huo utatumika kwa mikutano ya amani.
Hayo yanajiri huku Muungano huku muungano huo ukiwateua Brian Mbugua na Anthony Mwaura kuelekea Ugiriki kushuhudia uchapishaji wa karatasi za kupigia kura.
Already have an account? Login