Serikali yaanza kutoa chanjo dhidi ya yellow Fever

Serikali imeanza rasmi kutoa chanjo dhidi ya homa ya manjano yaani yellow Fevor kwa wakazi wa Kaunti ya Isiolo na Garissa.

Wizara ya Afya imezindua kampeni hiyo leo hii  huku ikilenga hasa maeneo la Merti na Garbatula kwenye Kaunti ya Isiolo na Lagdera, Balambala katika Kaunti ya Garissa ambapo takriban  watu elfu mia saba wanatarajiwa kuchanjwa.

Akizungumza mjini Garissa alipoongoza kampeni hiyo, Kaimu Mkurugenzi Matibabu wa Wizara ya Afya Daktari Patrick Amoth amesema wanaolengwa ni watu wote, kuanzia watoto wa miezi tisa hadi wazee wenye umri wa miaka sitini.